Mradi wa Safe Mobility ni ushirikiano kati ya Akron Children’s Hospital na Goodyear Foundation. Huwezesha hospitali na mashirika ya kushirikiana na jamii kupanua mipango ya usalama wa mtoto inayolenga viti vya mtoto msafiri, kofia za baiskeli, na madereva watoto.

Usalama wa Mtoto Msafiri

Kiti cha gari ni mojawapo ya vitu muhimu ambavyo utanunua kwa ajili ya usalama wa mtoto wako, lakini pia kinaweza kuwa mojawapo ya vitu vya kutatiza. Zaidi ya 70% ya viti vya gari vinavyowekwa na familia vina angalau shida moja kubwa ya uwekaji. Tumia kifaa cha kuchagua kiti cha gari kwenye ukurasa huu kwa msaada wa kuchagua kiti cha gari kifaacho kwa mtoto wako, na angalia video zilizochini ya ukurasa huu kwa vidokezo vya uwekaji unaofaa wa kiti cha gari.

Watoto wote chini ya umri wa 13 wanafaa kusafiri kwenye kiti cha nyuma cha gari. Mifuko ya hewa ya kiti cha msafiri mbele ya gari ni ya nguvu na inaweza kusababisha majeraha makubwa kwa watoto chini ya umri wa 13.

Wasiliana na Akron Children's Hospital ili kujibu maswali na kupokea msaada wa kitaalamu kuhusiana na uchaguzi na uwekaji wa kiti kupitia (330) 543-8942.

Kipindi kinachojulikana kama "Siku 100 za Mauti Zaidi" kwa madereva wachanga, wasio na uzoefu huanzia Siku ya Kumbukumbu hadi Siku ya Wafanyakazi. Wakati huu, zaidi ya asilimia 30 ya vifo vinavyohusisha madereva vijana hutokea. Madereva wasio na uzoefu mara nyingi hudhihirisha tabia hatari za uendeshaji - kama vile kuendesha kwa mwendo wa kasi, kuendesha gari wakiwa na usingizi , kutojifunga mikanda ya usalama kila wakati, na husumbuliwa kwa urahisi – hasa ikiwa marafiki zao wako kwenye gari.

Vidokezo kwa madereva wapya:

  • #1 Usikubali kusumbuliwa na vitu kama vile simu za mkononi.
  • #2 Usiendeshe gari kwa kasi. Thuluthi moja ya ajali zinazowahusisha vijana zinatokana na kuendesha gari kwa kasi.
  • #3 Hakikisha kuwa kila mtu kwenye gari amefunga mkanda wa usalama!
  • #4 Punguza uendeshaji gari usiku. Miongoni mwa ajali za usiku zinazowahusisha vijana, asilimia 57 hutokea kati ya saa 9 usiku na saa sita usiku.

Ushauri kwa wazazi:

  • Jambo moja muhimu zaidi ambalo wazazi wanaweza kufanya ili kuwalinda vijana wao wanaoendesha gari ni kuhusika kikamilifu wakati kijana anapojifunza kuendesha gari.
  • Zungumza na vijana mapema na mara kwa mara kuhusu kujiepusha na tabia hatari, kama vile kuendesha gari kwa kasi, kutokuwa waangalifu na kusumbuliwa wakati wa kuendesha gari.
  • Zungumza na vijana wako kuhusu kuwa waangalifu kwa makosa ya madereva wengine.
  • Wafunze kwa kuwa kielelezo. Usikaribie magari mengine sana, rekebisha kasi yako kulingana na hali na upunguze tabia hatari unapoendesha gari.
  • Weka makubaliano ya uendeshaji gari kati ya mzazi na kijana ambayo hubainisha kanuni za familia kwa madereva vijana.

Jinsi ya kuweka kiti cha mtoto mdogo
Jinsi ya kuweka kiti kinachobadilishwabadilishwa/kinachounganishwa
kiti cha kugeuzwa na mtoto wako mchanga
Jinsi ya kuweka kiti cha busta

Usalama wa Baiskeli

Kuendesha baiskeli ni njia bora ya watoto kuwa wachangamfu na kucheza nje ya nyumba! Fuata vidokezo hivi ili kuhakikisha kwamba familia nzima inaendesha kwa usalama.

Katika Akron, pamoja na miji mingine mingi, watoto chini ya umri wa 16 wanahitajika kuvalia kofia ya helmeti wakati wanaendesha baiskeli. Wazazi: Onyesha tabia nzuri! Mtoto wako ataamua kuchagua kuvalia kofia ya helmeti iwapo unavalia moja pia.

Angalia video iliyochini ya ukurasa huu ili kuhakikisha baiskeli yako ni salama na tayari kuendeshwa!

Iwapo baiskeli ya mtoto wako ina uharibifu mkuu, maduka mengi ya baiskeli hutoa huduma za urekebishaji. Iwapo uharibifu ni mdogo, vituo vya umma vya kurekebisha baiskeli vinaweza kupatikana kwenye Ohio Erie Canalway katika sehemu zifuatazo:

  • Summit Lake – kwenye Towpath
  • Park East – kwenye Towpath
  • Richard Howe House – kwenye Towpath
  • Lock 3 – kwenye muunganisho wa Towpath
  • Mustill Store – kwenye Towpath
  • Northside Station – kwenye kijia cha kuunganisha Towpath
  • Rubber Ducks Stadium - kwenye Main St.
  • Summit County Library – Tawi la Downtown
  • Barabara ya Akron Zoo

Watoto zaidi ya umri wa 12 wanafaa kuendesha baiskeli zao barabarani badala ya njia ya kutembea kwa miguu. Watoto chini ya umri wa miaka 10 wana uwezo mdogo kuliko watoto wakubwa wa kuamua kasi ya barabarani, ambao huwaweka kwenye hatari kubwa ya ajali barabarani. Kabla ya kuwaruhusu watoto wakubwa kuendesha barabarani, wafundishe kuhusu usalama wa baiskeli na ishara za barabarani.

Helmet Example 1
Helmet Example 2
Helmet Example 3
Helmet Example 4

Ili kuwa salama unapoendesha baiskeli au skuta, ni muhimu kuhakikisha kwamba watoto wote (na watu wazima) wanavaa helmeti inayowatoshea vizuri. Shanga, pinde, vishungi, klipu, vitambaa vya kufunika kichwani na mashungi ya nywele yanaweza kuzuia helmeti, kwa hivyo timu yetu ya Safe Mobility ilishirikiana na baadhi ya wataalam kubuni baadhi ya mapendekezo ili kurahisisha kuvaa helmeti.

Wakati mwingine suluhisho ni rahisi kama kutumia helmeti kubwa zaidi. Nyakati nyingine, marekebisho machache yanaweza kuleta tofauti.

  • Hakikisha fundo la nywele na mashungi ya nywele yako karibu na ukosi wa shingo.
  • Ongeza shanga na klipu chini ya sehemu ya helmeti.
  • Pini mbili za kufungia zinapaswa kuondolewa au kuwekwa chini ya sehemu ya helmeti.
  • Ongeza kifunika kichwa, kofia ya satini au skafu ya hariri ili kulinda nywele.
  • Kama wazazi, valia helmeti yako kila wakati unapopanda ili kuwa kielelezo.

Kukaza Helmeti:

  1. Chagua helmeti inayotoshea vizuri — kuna za ukubwa mbalimbali.
  2. Valia helmeti, kuanzia nyuma ya kichwa.
  3. Helmeti inapaswa kutoshea vizuri kichwani pako.
  4. Weka kwa uangalifu na uimarishe kwa vitanzi. Rekebisha vitanzi ikihitajika. Ni vizuri ikaze lakini isikaze kiasi kwamba huwezi kugeuza kichwa chako.
  5. Helmeti huwekwa ipasavyo wakati umeacha upana wa vidole 2 pekee kati ya nyusi zako na helmeti.

Vidokezo vya Usalama wa Baiskeli


Valia kofia ya helmeti na nguo zifaazo

Angalia pumzi kwenye magurudumu yako

Angalia breki zako

Hakikisha mnyororo na mpini zinafanya kazi vyema


Kwa maelezo zaidi kuhusu usalama wa baiskeli na kofia ya helmeti, piga simu kwenye laini ya Akron Children’s Hospital Injury Prevention: (330) 543-8942.

Video ya Usalama wa Baiskeli

Uendeshaji Salama wa Mtoto

  • Sheria za Leseni ya Dereva Aliyehitimu za Ohio hupunguza hatari ya ajali ya mtoto
  • Imekadiriwa kwamba 1 kati ya ajali 4 zimesababishwa na uendeshaji uliochachawizwa (k.v. utumiaji wa simu ya rununu)
  • Mwendo kasi ni sababu ya ajali mbaya 1 kati ya 3 za gari
  • Hatari ya ajali ya mtoto imeongezeka kwa 44% kwa kuongeza msafiri 1, huongezeka mara mbili kwa kuongeza wasafiri 2 na mara nne kwa kuongeza wasafiri 3 au zaidi
  • Wazazi ndio washawishi namba 1 kwenye uendeshaji salama wa watoto wao
Nitafanya tabia salama za uendeshaji na kutii sheria za Leseni ya Dereva Aliyehitimu za Ohio kwa

  • Kufunga mkanda wangu wa usalama
  • Kutii sheria za amri ya kutotoka nje (isipokuwa kwa sababu za shule, za kazi au za kidini)
  • Kuendesha kulingana na kiwango cha mwendo kasi
  • Kuepuka uendeshaji wa kinguvu, kama vile kuwafanya wengine kwenda haraka, kuingia na kutoka kwenye laini za barabara, na kupuuza ishara za trafiki
Nitaweka simu yangu mbali wakati ninapoendesha. Nitapangilia GPS yangu na muziki kabla ya kuanza safari.

Iwapo ninahisi utofauti kwa sababu ya pombe, dawa za kulevya, matibabu, hisia kali au ukosefu wa usingizi, sitaendesha gari langu. Badala yake, nitajaribu kuwasiliana na dereva mwingine anayeendesha kwa usalama.

Nitaendesha nikiwa na mtu 1 asiyekuwa wa familia (chini ya 21) kwa mwaka wangu wa kwanza wa uendeshaji, isipokuwa akiambatana na mzazi au mlezi.

  • Ninaelewa kwamba kuwa na wasafiri wengi kunamaanisha uchachawizi mwingi
  • Wakati nikiendesha nikiwa na wasafiri kwenye gari, nitaweka makini yangu kwenye barabara na kuwauliza wasafiri kupunguza uchachawizi wakati ninapoendesha
Ninaahidi kufuata sheria za makubaliano haya, na ninaelewa adhabu (urekebishaji wa kisheria na wa nyumbani) iwapo sifuati.

Kama mzazi, ninaahidi kuonyesha tabia salama. Ninaelewa mtoto wangu ananitegemea kumfundisha jinsi ya kuendesha salama.


Kwa kutumia tovuti hii, unakubali kutumia vidakuzi vyetu. Ili kupata maelezo zaidi, soma sera ya faragha ya Akron Children.

,